Sababu zinazomfanya Dkt.Mwinyi kupewa kipaumbele zaidi katika Uchaguzi wa kesho

NA DIRAMAKINI 

NI dhairi kuwa, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameonesha uongozi imara na dira ya maendeleo kwa Zanzibar kupitia utekelezaji wa miradi mikubwa ya kiuchumi na kijamii.
Aidha,kupitia Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050, serikali yake imeboresha miundombinu ya barabara, bandari na viwanja vya ndege, hatua iliyochochea ukuaji wa sekta ya utalii na biashara.

Pia,Dkt.Mwinyi amefanikisha ujenzi na ukarabati wa hospitali, vituo vya afya na shule, akisisitiza upatikanaji wa huduma bora za kijamii kwa wananchi wa mijini na vijijini.

Katika nyanja za kiuchumi, Dkt.Mwinyi amesimamia mageuzi makubwa ya kiutawala na uwekezaji, ikiwemo kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kupitia Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).

Uanzishaji wa maeneo maalum ya kiuchumi kama vile Micheweni Free Economic Zone na uendelezaji wa sekta ya mafuta na gesi umekuwa chachu ya ajira kwa vijana na ongezeko la mapato ya serikali.

Vilevile, juhudi zake za kupambana na rushwa na kuongeza uwazi katika matumizi ya rasilimali za umma zimeimarisha imani ya wananchi kwa serikali.

Kwa misingi hiyo, Dkt.Hussein Ali Mwinyi anafaa kuchaguliwa tena kutokana na ufanisi aliouonesha katika kuleta mageuzi ya kiuchumi, kijamii na kiutawala ili miaka mitano ijayo iwe ya neema zaidi Zanzibar.

Uongozi wake umejikita katika umoja, uwajibikaji na maendeleo jumuishi, akilenga kujenga Zanzibar yenye uchumi wa kisasa na ustawi wa wananchi wote huku amani kote Unguja na Pemba ikiwa msingi muhimu.

Hivyo, kuendelea kwake madarakani inamaanisha mwendelezo wa sera zenye tija, utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, na kuimarika kwa amani na utulivu, ambazo ni nguzo za maendeleo endelevu.

Kesho Oktoba 29,2025 ni siku muhimu sana katika historia ya taifa letu, ni siku ya uchaguzi, ni siku ambayo sauti yako ina thamani kubwa kuliko siku nyingine yoyote.

Vijana,wanawake, wazee wote waliotimiza vigezo vya Tume ya Uchaguzi kila mmoja wetu ana nafasi muhimu kesho.

Hivyo, amka mapema, nenda kituoni,fuata taratibu,mpigie Dkt.Hussein Ali Mwinyi kura yako kwa amani, kisha urudi nyumbani ukiwa na fahari kuwa umetimiza wajibu wako kama raia mzalendo.

Kumbuka kuwa,Taifa letu linahitaji sauti yako,amani ni jukumu letu sote,maendeleo yanatokana na ushiriki wetu na Dkt.Hussein Ali Mwinyi anatosha Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news