Tanzania yaimarisha matumizi ya TEHAMA katika ujifunzaji

DODOMA-Serikali inaendelea kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ujifunzaji na ufundishaji katika ngazi zote za elimu nchini kuanzia elimu ya awali hadi vyuo vikuu.
Hayo yameelezwa tarehe 16 Oktoba 2025 na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Hussein Mohamed Omar alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Imagine World Tanzania Dkt. Jacqueline Mgumia katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.
Dkt. Omar ameongeza kuwa, Wizara tayari imeandaa Mkakati wa Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali katika Elimu sambamba na miongozo ya kitaifa ya elimu kidigitali katika ngazi ya Elimu msingi, Elimu ya Ufundi na Elimu ya Juu ambapo amesisitiza kuwa, kupitia mikakati hiyo Tanzania inaendelea kupiga hatua kubwa katika matumizi ya teknolojia kwenye sekta ya elimu nchini.
Kwa upande wake Dkt. Mgumia ameishukuru Wizara kwa kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo ambayo inatekeleza mradi wa kuwezesha matumizi ya TEHAMA katika kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili kwa ngazi ya elimu msingi.
Amesema, kupitia mradi huu unaotekelezwa katika mikoa 5 ya Tanzania Bara na 2 Zanzibar Shule 500 zitanufaika na mradi kwa kupatiwa vifaa (tablets) zenye programu za ujifunzaji ili kuongeza uelewa wa KKK. Mradi huu pia unatoa mafunzo kwa walimu na kufanya utafiti juu ya matokeo ya kufundisha kKK na matumizi ya TEHAMA katika madarasa ya awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news