DAR-Zoezi la upigaji kura linaendelea kwa amani na utulivu katika Jimbo la Temeke, hususan katika Kata za Vetinari, Tandika, na Makangarawe, ambapo wananchi wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo la kidemokrasia.
Katika Shule ya Msingi Yombo Dovya, wapiga kura wameonekana wakiwa katika foleni wakihakiki majina yao kabla ya kupiga kura, kisha kurejea majumbani mwao kwa utulivu mara baada ya kumaliza mchakato.
Hali kwa ujumla katika vituo hivyo ni shwari, na maandalizi yameonekana kuwa mazuri, huku maafisa wasimamizi wa uchaguzi wakihakikisha kila kituo kinaendesha zoezi kwa ufanisi.
Vikosi vya ulinzi na usalama vimeendelea kuwepo kuhakikisha amani na usalama vinatawala wakati wote wa upigaji kura.



