NA DIRAMAKINI
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa katika mikoa saba inayotarajiwa kunyesha kuanzia leo.
Mvua hiyo inatarajiwa katika katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (pamoja na visiwa vya Mafia), Morogoro na Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa ya TMA, hali kama hiyo pia inatarajiwa kuendelea hadi kesho Jumanne katika mikoa hiyo na kuongezeka hadi maeneo ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
Aidha,mamlaka imewataka wananchi kuchukua tahadhari na kufuatilia taarifa zitakazotolewa ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.
Tags
Habari
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Mvua Kubwa
Tanzania Meteorological Agency (TMA)
Utabiri wa Hali ya Hewa Tanzania

