Ujenzi wa Bwawa la Songwe lawakutanisha viongozi

DODOMA-Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,Mhandisi Mwajuma Waziri ameongoza kikao cha Katibu Wakuu kuhusu mjadala wa Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Songwe Chini pamoja na mtambo wa kuzalisha nishati ya umeme.
Kikao kimewakutanisha Katibu Wakuu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati pamoja na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe kimefanyika Wizara ya Maji jijini Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2025.
Viongozi hao wamekubaliana andiko la dhana ya mradi liwasilishwe katika mamlaka husika mapema.

Kukamilika kwa Bwawa hilo kutawanufaisha wananchi waishio ndani ya Bonde la Mto Songwe katika wilaya za Ileje, Kyela, Momba, Mbozi na Mbeya kwa kuwapatia umeme wa uhakika, maji kwa ajili ya umwagiliaji vilevile kwa ajili ya matumizi ya majumbani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news