LESENI ya udereva ni hati ya kisheria inayomruhusu dereva kuendesha chombo katika daraja lililooneshwa katika leseni hiyo.
Nchini Tanzania, leseni za udereva zimegawanywa katika madaraja mbalimbali kulingana na aina ya gari, uzito, na madhumuni ya matumizi au chombo chochote cha moto.
FUATA HATUA HIZI
HATUA 1:
Nenda Chuo cha Udereva kwa ajili ya Mafunzo ya Udereva. Ukimaliza mafunzo, fanya mtihani wa shule hiyo ya udereva ili kupata Cheti.
HATUA 2:
Anzisha Maombi ya Leseni kwenye mfumo wa Leseni za Udereva wa TRA. Mfumo huo Unaitwa IDRAS.
Ili kuufikia mfumo huo, kwanza hakikisha una namba ya Utambulisho wa Mlipakodi, yaani TIN, kisha fuata hatua zifuatazo:
1. Ingia Google andika TRA TAXPAYERS PORTAL. Ukurasa wa TRA ukishafunguka
2. Jisajili kwenye mfumo huo kwa Kuingiza Taarifa zako, ukianzia na TIN yako, kisha tengeneza Password. Utatumiwa namba ya Msimbo (code) ya kuhuisha (activate) usajili wako.
3. Ingia kwenye mfumo wa TRA kwa ku-log in kwa USER NAME yako ambayo ni TIN yako na Password Uliyoitengeneza.
4. Chagua MOTOR VEHICLES AND DRIVING LICENCES. Click hapo
5. Mfumo wa IDRAS utafunguka. Kwenye huo mfumo chagua palipoandikwa COMPUTERIZED DRIVING LICENCE
6. Kwenye APPLICATION TYPE, chagua PROVISIONAL kisha ingiza taarifa zinazotakiwa ikiwemo Mkoa, shule ya udereva uliosoma, picha, daraja la leseni unaloombea Provisional nk kisha SAVE.
7. Baada ya kumaliza kujaza maombi yako, utaenda TRA kwa ajili ya kupigwa picha na kuchukukiwa alama za vidole (finger print) pamoja na sahihi.
Baada ya hapo, Utapatiwa CONTROL number ambayo ukishalipia utapokea leseni yako ya PROVISIONAL au kwa jina jingine LENA.
HATUA 3: OMBA LESENI MPYA
Ukishakuwa na Leseni ya Lena sasa unaweza kuomba leseni mpya. Hadi hatua hii utakuwa tayari umeshajua kutumia mfumo maana tayari una akaunti kwenye mfumo na uliingia wakati unakata LENA.
Na kama hukuwa umekata wakati wa kusomea udereva basi utafanya vyote kwa pamoja, utakata lena ukimaliza utaanzisha maombi ya leseni. Fuata hatua zifuatazo:
1. Kwenye COMPUTERIZED DRIVING LICENCE tafuta palipoandikwa Application type, kisha chagua New. Kisha ingiza taarifa zako kama vile mkoa, wapi utapokelea leseni yako. Chagua daraja la leseni unalotaka, kituo cha polisi utakachofanyia test. Kisha hifadhi taarifa zako
2. Thibitisha EFD risiti yako. Baada ya hapo ukimaliza save. Utapokea bill yako ya kulipia ada ya kutestiwa na askari. Ukishalipia,nenda kituo cha polisi, Mtafute Mtahini au VECO kwa ajili ya test.
3. Ukimaliza test na kupass, rudi tena kwenye mfumo. Ingia kama ulivyoingia mwanzo, ukifika utakuta taarifa zako zimebadilika, kwenye competence test imekuwa PASS.
Na Bill yako ya leseni ambayo ni shilingi 70,000 utaikuta hapo. Utakachofanya ni kuiprint na kwenda kulipia tayari kwa kusubiri TRA wakuprintie leseni yako ukachukue.
4. Baada ya kama siku chache hadi wiki leseni yako itakuwa tayari. Mfumo utakutumia email au utapokea meseji kwenye simu yako inayoonesha leseni yako ipo tayari uende ukaichukue.
Ni imani yangu makala hii itakuwa imekuongezea uelewa wa namna ya kuomba leseni kwa mara ya kwanza. (RSA Tanzania)
