Kwa kumpigia kura,Dkt.Hussein Ali Mwinyi na CCM katika Uchaguzi Mkuu huu unathibitisha kuwa, unaunga mkono juhudi zake za kuimarisha uchumi, kuboresha huduma za kijamii na kulinda amani ya nchi. Kura yako ni msingi wa kuimarisha kasi ya maendeleo Zanzibar kwa ustawi bora wa jamii na Taifa kwa ujumla.Hakika, imani yetu ni kubwa kwa Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi na tunampa miaka mitano tena ili atuongoze.
