DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na kuzungumza na Balozi wa Jamhuri ya Burundi nchini Tanzania, Mhe. Leontine Nzeyimana, katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Burundi.



