Waziri Kombo apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Iran

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amepokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini, Mhe. Mohammad Javad Hemmatpanah, katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Kombo amempongeza Mhe. Hemmatpanah kwa uteuzi wake na kumhakikishia ushirikiano wa karibu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika utekelezaji wa majukumu yake nchini.
Waziri Kombo amebainisha kuwa, Tanzania na Iran zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu na wa kirafiki, uliojengwa juu ya misingi ya kuheshimiana na maslahi ya pamoja. 

Ameongeza kuwa,uhusiano huo unaendelea kuimarika katika maeneo mbalimbali yakiwemo biashara na uwekezaji, elimu na afya, nishati,sayansi, teknolojia na ubunifu.
Kwa upande wake, Balozi Mteule Mhe. Hemmatpanah alieleza dhamira ya Serikali ya Iran kuendelea kupanua wigo wa ushirikiano na Tanzania katika sekta za uchumi na uwekezaji, dawa na famasia, pamoja na uendelezaji wa miundombinu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news