Waziri Mkuu kumwakilisha Rais Dkt.Samia uapisho wa Rais mteule wa Seychelles

VICTORIA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 26, 2025 amewasili Seychelles kwa ajili ya kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho wa Rais mteule wa sita wa nchi hiyo Dr. Patrick Herminie.
Tume ya Uchaguzi ya Taifa ilimtangaza Mheshimiwa Dkt. Patrick Herminie wa Chama cha United Seychelles (US) kuwa mshindi baada ya kumbwaga Rais aliyekuwa madarakani, Mheshimiwa Wavel Ramkalawan wa Chama cha Linyon Demokratik Seselwa (LDS).
Mheshimiwa Dkt. Patrick Herminie alipata asilimia 52.7% ya kura, huku Rais Wavel Ramkalawan akimaliza wa pili kwa kupata 47.3% ya kura.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news