Wizara ya Fedha yahimiza watumishi kushiriki michezo

DODOMA-Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo amesema kuwa, watumishi wa Wizara ya Fedha wataendelea kushiriki katika michezo mbalimbali ili kujenga afya, akili na ushirikiano.
Bi.Omolo ameyasema hayo jijini Dodoma alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Capital City Marathon Dodoma, Bw. Nsolo Mlozi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Marathon Oktoba 5, 2025.

Kwa upande wake Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Capital City Marathon Dodoma, Bw. Nsolo Mlozi alisema, wameendelea kuwa wabunifu kila mwaka ili kuwavutia wadau wengi zaidi kushiriki mbio hizo.
Aidha,ameishukuru Wizara ya Fedha kwa kuwaruhusu watumishi wake kushiriki kwa idadi kubwa katika mbio hizo na akaahidi kuhakikisha usalama kwa wote wanaotarajia kushiriki kwa kuwa ndio kipaumbele cha kwanza katika jambo hilo.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo, Bi. Scola Malinga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news