ZMA yateta na manahodha wa Mkokotoni Pangani

ZANZIBAR-Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) imekutana na Ushirika wa Manahodha wa Mkokotoni Pangani kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuwapatia vifaa vya usalama kwa ajili ya shughuli zao za kila siku baharini.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho cha siku moja cha mashauriano, Mkurugenzi wa Ulinzi, Usalama na Mazingira ya Bahari wa ZMA, Kepteni Khamis Taji Khamis, amesema jukumu kuu la Mamlaka hiyo ni kuhakikisha usalama wa shughuli zote za usafiri baharini pamoja na kulinda mazingira ya bahari.

Kepteni Taji aliwapongeza Manahodha wa Ushirika huo kwa hatua yao ya kununua chombo maalum kwa ajili ya shughuli za uokozi, akikitaja kuwa ni kitendo cha kizalendo. 

Aliahidi kuwa ZMA itaendelea kushirikiana nao kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande wake, Katibu wa Ushirika huo, Ahmada Haji Kombo (maarufu kama Gora), aliomba ZMA kuanzisha kozi maalum za mafunzo ya wiki mbili hadi tatu kwa Manahodha wa maeneo ya Zanzibar, ili kuwajengea uwezo bila kulazimika kusafiri hadi Tanzania Bara kwa masomo hayo, jambo ambalo limekuwa changamoto kwao kutokana na majukumu ya kila siku.

Manahodha wengine waliopata fursa ya kuzungumza – akiwemo Haji Ame Ameir (Tumbatu Jongoe), Kombo Ali Kombo (Tumbatu Kichangani), na Juma Jaku Kitiba – walieleza kuwa bado kuna uelewa mdogo kwa baadhi ya abiria wanaosafiri kati ya Mkokotoni na Tumbatu kuhusu umuhimu wa kuvaa life jacket. Walipendekeza ZMA kufanya ziara maalum Tumbatu kwa ajili ya kutoa elimu ya usalama baharini kwa wananchi.

Naye Msimamizi Mkuu wa ZMA Kanda ya Kaskazini Unguja, Simai Nyange Simai, alieleza mafanikio yaliyopatikana kwa kushirikiana na Manahodha hao, ikiwa ni pamoja na usajili wa vyombo, utoaji wa vitambulisho vya mabaharia na uendeshaji wa shughuli za uokozi wakati wa ajali baharini.

Simai aliushukuru uongozi wa Ushirika wa Manahodha kwa ushirikiano na juhudi zao katika kulinda maisha ya abiria na mali zao.

Kwa ujumla ZMA inaendelea na utaratibu wa kuwatembelea na kuwasikiliza Manahodha na Mabaharia katika maeneo yote ya Unguja na Pemba, ikiwa ni pamoja na kuwapatia msaada wa vifaa vya uokozi, kutoa elimu ya usalama na kushughulikia changamoto zao kwa lengo la kuimarisha

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news