BoT yashiriki Mkutano wa Mwaka wa Taasisi za Fedha Afrika (AFIS) jijini Casablanca

CASABLANCA-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeshiriki katika Mkutano wa Mwaka wa Taasisi za Fedha Afrika (AFIS) uliofanyika jijini Casablanca, Morocco, kuanzia tarehe 3 hadi 4 Novemba 2025.
Mkutano huo uliwakutanisha viongozi wakuu na wadau muhimu wa sekta ya fedha kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika.

BoT iliwakilishwa na Naibu Gavana, Dkt. Yamungu Kayandabila, ambaye alishiriki kama mtoa mada katika mjadala uliolenga kujadili nafasi ya benki za ndani barani Afrika katika usimamizi wa akiba ya fedha za kigeni.
Katika mchango wake, Dkt. Kayandabila alibainisha umuhimu wa kupitia upya vigezo vinavyotumika kupima ukwasi na uhimilivu wa mabenki ya ndani, akisisitiza kwamba kufanya hivyo kutaziwezesha benki hizo kuaminika zaidi na kushiriki kikamilifu katika kusimamia sehemu ya akiba ya fedha za kigeni za nchi zao.

Wakati wa mkutano huo, Dkt. Kayandabila pia alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika (BOA), Bw. Amine Bouabid, ambapo walijadili fursa za ushirikiano na njia za kuboresha huduma za fedha nchini Tanzania.
Ushiriki wa Benki Kuu katika mkutano huo unaakisi dhamira yake ya kuendeleza ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika masuala ya kifedha, pamoja na kuimarisha usimamizi endelevu wa akiba ya fedha za kigeni barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news