DAR-Rais wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini Comoro (Chambre anti-corruption),Bi Fahamoue Youssouf akiambatana na maafisa wake amewasili Dar es salaam kwa ziara ya kikazi kwa mwaliko wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),ndugu Crispin Chalamila.

Ziara hiyo imeratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro ambapo Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Balozi Saidi Yakubu aliwakaribisha Tanzania na kuwaeleza namna ziara hiyo itakavyokuza ushirikiano katika eneo la utawala bora.



