Dkt.Samia Suluhu Hassan aapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

DODOMA-Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Novemba 3,2025 ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. George Mcheche Masaju kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Tukio hilo linaashiria kuanza kwa Muhula Mpya wa Uongozi wake utakaodumu hadi mwaka 2030, baada ya ushindi wa kura wa zaidi ya asilimia 97 kulingana na matokeo yaliyotangazwa hivi karibuni na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kutokana na Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29,2025.
Katika hatua nyingine,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wa mikoa na wilaya kuhakikisha maisha ya wananchi yanarejea katika hali ya kawaida kuanzia leo Novemba 3, 2025.

Amesema, Serikali itaendelea kulinda amani, umoja na ustawi wa wananchi, huku akisisitiza kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vina jukumu kubwa la kuhakikisha nchi inarejea katika hali ya utulivu na shughuli za kijamii na kiuchumi zinaendelea kama kawaida.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi wameapishwa rasmi leo kuongoza Taifa la Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Aidha, zoezi hilo limezingatia takwa la kisheria kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, George Mcheche Masaju na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news