Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limemteua Meneja Mashindano wa TFF, Baraka Kizunguto kuwa Mratibu (General Coordinator) wa michezo ya nusu fainali ya hatua za awali kufuzu Kombe la Dunia Kanda ya Afrika (Play-Off Tournament) kati ya Nigeria vs Gabon na fainali. Michezo hiyo itachezwa Rabat, Morocco Novemba 13 na Novemba 16,2025.
