SERIKALI imeendelea kuboresha elimu kupitia matumizi ya TEHAMA kwa kuwajengea uwezo walimu wa shule za umma nchini. Kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), hadi kufikia Desemba 2024, walimu 3,798 kutoka shule 1,791 za Serikali za Tanzania Bara na Zanzibar wamepatiwa mafunzo ya TEHAMA.
Mafunzo haya, yanayoratibiwa na Serikali kupitia UCSAF kwa ushirikiano na vyuo vikuu vya UDOM, MUST, na DIT, yamelenga kuwawezesha walimu kutumia teknolojia katika ufundishaji na kutatua changamoto ndogo za vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa na Serikali kupitia UCSAF katika shule wanazofundisha.
Hatua hii ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha elimu bora, jumuishi na yenye kuendana na mahitaji ya karne ya kidigitali.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


























