SHIRIKA la Umeme Zanzibar (ZECO) limetangaza kuwa kutakuwa na maboresho ya miundombinu katika baadhi ya maeneo kesho, Jumapili, tarehe 16, 2025. Kazi hizo zitahusisha uhamishaji wa nguzo za umeme wa msongo wa kilovolti 33 na 11.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, lengo la uamuzi huo ni kuwarahisishia kazi wakandarasi wa ujenzi wa barabara za juu (fly over) unaoendelea katika maeneo ya Amani na Mwanakwerekwe.
Kutokana na maboresho hayo, Shirika la Umeme litalazimika kuzima umeme wa njia za msongo wa kilovolti 33 na 11 ili kupisha utekelezaji wa kazi hiyo.








Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






