FAMILIA ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, hayati Raila Odinga, imeingia tena katika majonzi kufuatia kifo cha mmoja wa wanafamilia wake, Beryl Achieng’ Odinga.
Taarifa za msiba huo zilitolewa Jumanne, Novemba 25, na dada yake marehemu, Ruth Odinga, ambaye alithibitisha kutokea kwa kifo hicho lakini hakutaja chanzo chake.
Ruth alieleza kuwa familia imepokea msiba huo kwa majonzi makubwa, ikisisitiza kuwa wanakubali mapenzi ya Mungu katika kipindi hiki kigumu.
“Ni kwa moyo mzito lakini tukikubali mapenzi ya Mungu, tunatangaza kifo cha ghafla cha Beryl Achieng’ Odinga. Binti wa marehemu Jaramogi Oginga Odinga na Mama Mary Ajuma Oginga. Mama yake Ami Auma, Chizi na Taurus,” alisema Ruth katika taarifa yake.
Beryl Achieng’ Odinga, ambaye anatoka katika ukoo wenye ushawishi mkubwa kisiasa nchini Kenya, amekuwa nguzo muhimu ndani ya familia hiyo, na kifo chake kimetajwa kuwa pigo kubwa kwa wapendwa wake.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
























