SOKO la Bidhaa Tanzania (TMX) limefanikiwa kuuza korosho ghafi tani 26,254 za wakulima wanaounganishwa kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha TANECU Ltd katika mnada wa kwanza wa zao la korosho uliofanyika mkoani Mtwara.
Katika mnada huo, korosho ziliuzwa kwa bei ya juu ya Shilingi 3,520 na bei ya chini ya Shilingi 2,550 kwa kilo, kupitia mfumo wa kidijitali wa TMX unaolenga kuhakikisha uwazi, ushindani, na tija kwa mkulima.
Katika mnada huo, korosho ziliuzwa kwa bei ya juu ya Shilingi 3,520 na bei ya chini ya Shilingi 2,550 kwa kilo, kupitia mfumo wa kidijitali wa TMX unaolenga kuhakikisha uwazi, ushindani, na tija kwa mkulima.Taarifa zinaeleza kuwa korosho hizo zilikuwa na jumla ya mafungu (loti) 105, ambapo mzigo wote uliuzwa kwa mafanikio kupitia mfumo wa soko la bidhaa, hatua inayotajwa kuashiria mwanzo mzuri wa msimu mpya wa mauzo ya korosho mwaka 2025/2026.
Akizungumza baada ya mnada huo, Mwenyekiti wa TANECU Ltd, Karim Chipola, ameipongeza Serikali kwa kuanzisha mfumo wa TMX, akisema umeleta mapinduzi makubwa katika biashara ya mazao nchini.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo









