ZANZIBAR-Wajumbe wa Baraza la Kumi na Moja la Wawakilishi Zanzibar wamemchagua Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid kuwa Spika wa baraza hilo kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2030.
Katika uchaguzi huo,Mheshimiwa Zubeir amepata kura 56 kati ya kura 68 zilizopigwa sawa na asilimia 94.6.Spika Zubeir hii ni awamu yake ya tatu ya kuongoza baraza hilo ambapo amechukua Spika tokea Baraza la Tisa.
