Mwanajeshi wa Marekani akamatwa akiingia Tanzania kupitia mkoani Mara akiwa na mabomu

MARA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Polisi Tarime na Rorya limesema Jumapili ya November 16, 2025 saa sita mchana katika eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya wa Sirari limemkamata Charles Onkuri Ongeta (30), mwenye uraia pacha wa Marekani na Kenya, Mwanajeshi wa Jeshi la Marekani Mwenye cheo cha Sajenti akiwa na mabomu manne aina ya CS M68 ya kurushwa kwa mkono.
Huu ni mfano wa mabomu ya kurusha kwa mkono.Picha na Mtandao.

Taarifa ya Polisi imeeleza kuwa,wamemkamata Charles akitokea Nchini Kenya kuingia Tanzania kwa kutumia gari yenye namba za usajili KDP 502 Y aina ya Toyota Landcruiser na kwamba kwa mujibu wa sheria ya umiliki wa silaha hata kama angeomba kibali cha kuingia nayo nchini asingeruhusiwa.

“Ushahidi unaendelea kukusanywa sambamba na kuhojiwa kwa tuhuma hizo ili hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news