ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na viongozi pamoja na wananchi mbalimbali katika Mazishi ya Marehemu Bibi Siena Mzee Muhammed aliyefariki leo tarehe 25 Novemba 2025.
Mapema, Rais Dkt. Mwinyi alijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Jeneza iliyosaliwa Masjid Twayyib uliopo Fuoni.
Marehemu Bibi Siena ni Bibi wa Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa.Marehemu amezikwa katika Makaburi ya Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi.







