ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemteua tena Dkt. Mwinyi Talib Haji kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
Uteuzi huu unaanza rasmi tarehe 4 Novemba 2025, huku Dkt. Haji kuapishwa rasmi siku ya Alhamisi, tarehe 6 Novemba 2025, saa 10:00 asubuhi Ikulu, Zanzibar.

