ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar ma Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Novemba 24,2025 ameongoza Kikao Kazi kilichowajumuisha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, kilichofanyika Ikulu, Zanzibar. 

Kikao Kazi hicho ni cha kwanza tangu Kipindi cha Pili cha Serikali ya Awamu ya Nane kuingia madarakani.

















