SONGWE-Katika kuimarisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imeendelea kutoa elimu kwa wadau muhimu wanaoshiriki moja kwa moja katika kuhakikisha usalama wa mipaka na safari za anga.
Elimu hii imetolewa kwa maafisa, wahudumu na wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Songwe (Mbeya) pamoja na Uwanja wa Ndege wa Iringa.
Jumla ya wahudumu 101 wamepatiwa elimu inayohusu tatizo la dawa za kulevya, ikijumuisha mbinu za kisasa za ufichaji wa dawa (concealment methods) zinazotumiwa na wasafirishaji kupitia viwanja vya ndege, pamoja na dalili na viashiria muhimu vya kuwatambua watu wanaoweza kujihusisha na biashara au usafirishaji wa dawa za kulevya.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)








