Rais Dkt.Mwinyi awaongoza viongozi na wananchi katika maziko ya mwanasiasa mkongwe Ali Ameir Muhammed

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewaongoza viongozi na wananchi mbalimbali katika maziko ya aliyekuwa mwanasiasa mkongwe marehemu Ali Ameir Muhammed, aliyefariki usiku wa kuamkia leo tarehe 26 Novemba 2025.
Marehemu Ali Ameir alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam.

Mapema, Rais Dkt. Mwinyi alijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Jeneza iliyosaliwa Msikiti wa Donge Kichamvyaani, Mkoa wa Kaskazini Unguja, pamoja na kutoa mkono wa pole kwa Wanafamilia, Ndugu na Jamaa wa Marehemu.
Dkt. Mwinyi amewataka kuwa na uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba mzito.

Wakati wa uhai wake, Marehemu Ali Ameir aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Jimbo la Donge, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Magharibi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Mhariri wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, pamoja na kuwa Mjumbe wa Baraza la Wadhamini CCM Taifa.
Marehemu Ali Ameir alizaliwa tarehe 5 Januari 1943 Donge Vijibweni. Ameacha Mke na Watoto 10. Mazishi yake yamefanyika kijijini kwao Donge Mbiji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here