ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kutangaza rasmi Baraza Jipya la Mawaziri katika hafla fupi itakayofanyika Ikulu Zanzibar, kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Hafla hiyo itahudhuriwa na wahariri pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, ambapo Rais Dkt. Mwinyi atalitambulisha Baraza hilo pamoja na wizara zake. Tukio hilo pia litangazwa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari nchini.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi atazungumzia mwelekeo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza vipaumbele vyake, vikiwemo Uchumi wa Buluu, Uwekezaji, Huduma za Jamii, Miundombinu, na Maendeleo Jumuishi kwa Wananchi.
Mawaziri watakaoteuliwa wataapishwa siku ya Jumamosi ya Novemba 15, 2025 saa 8:00 mchana, katika viwanja vya Ikulu Zanzibar ikiwa ni hatua muhimu inayoashiria mwanzo wa safari ya Kipindi cha Pili cha Serikali ya Awamu ya Nane.

