DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuapisha Mhe. Hamza Said Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bw. Hamza Said Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 05 Novemba, 2025.
Bw. Hamza Said Johari akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Samia (hayupo pichani) kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 05 Novemba, 2025.
Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uapisho wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Hamza Said Johari, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 05 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Hamza Said Johari, mara baada ya tukio la uapisho, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 05 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emanuel Nchimbi katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Hamza Said Johari, mara baada ya tukio la uapisho, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 05 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine baada ya kumuapisha Bw. Hamza Said Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 05 Novemba, 2025.Mhe. Hamza Said Johari ameapishwa rasmi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hafla iliyofanyika tarehe 5 Novemba, 2025 Ikulu jijini Dodoma.
Aidha, Mwanasheria Mkuu wa ameapishwa baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 3, Novemba 2025.



