NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Tume ya Uchunguzi, Sura ya 32, ameunda Tume huru ya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Dodoma na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Rais Dkt.Samia pia amemteua Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mohammed Chande Othman, kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Wajumbe wengine walioteuliwa ni Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania Profesa Ibrahimu Khamis,Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue , Balozi Radhia Msuya,
Balozi Gen. Paul Meela,IGP Mstaafu Said Mwema , Balozi David Kapya na aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC),Dkt.Stergomena Lawrence Tax