NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 66(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, amefanya uteuzi wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Walioteuliwa ni Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, Bw. Abdullah Ali Mwinyi, Balozi Khamis Mussa Omar pamoja na Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho.
