Tanzania yapongezwa matumizi ya viwango vya Kimataifa vya uhasibu sekta ya umma

NA BENNY MWAIPAJA
ACCRA GHANA

TANZANIA imepongezwa kwa kuwa miongoni mwa nchi kinara barani Afrika kutumia viwango vya kimataifa vya Uhasibu wa Sekta ya Umma (IPSAS), hatua iliyochangia kuweka uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za umma.
Mhasibu Mkuu wa Serikali -Tanzania, CPA. Leonard Mkude (kulia), akimkabidhi zawadi Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mauritania, Bw. Sachidanund Ramparsad, baada ya kutamatika kwa mjadala wao uliozungumzia namna Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa Sekta ya Umma (International Public Sector Accounting Standards-IPSAS) vinavyoweza kuchochea msukumo wa kisera na kutumia Uhasibu wa Ujumuishaji kwa Uboreshaji wa Usimamizi wa Mali na Madeni, wakati wa Mkutano wa Tatu wa Jumuiya ya Wahasibu wa Serikali barani Afrika, wenye kaulimbiu ya Afrika ya Kesho: Kuimarisha Usimamizi wa Fedha za Umma kwa ajili ya ustawi wa kiuchumi, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Accra (AICC), nchini Ghana.

Pongezi hizo zimetolewa mjini Accra, Ghana na Mshauri wa masuala ya matumizi ya viwango vya kimataifa vya uhasibu kutoka Zimbabwe, Bw. Amon Dhlimayo, wakati akitoa mada kuhusu matumizi ya viwango hivyo katika Mkutano wa Tatu wa Wahasibu wa Serikali Barani Afrika (African Association of Accountants General Meeting (AAAG), unaofanyika nchini humo.
Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Tanzania, CPA. Leonard Mkude (kulia), akizungumza wakati wa mjadala uliozungumzia namna Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa Sekta ya Umma (International Public Sector Accounting Standards-IPSAS) vinavyoweza kuchochea msukumo wa kisera na kutumia Uhasibu wa Ujumuishaji kwa Uboreshaji wa Usimamizi wa Mali na Madeni, wakati wa Mkutano wa Tatu wa Jumuiya ya Wahasibu wa Serikali barani Afrika, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Accra (AICC), nchini Ghana. Mjadala huo uliwahusisha pia Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mauritania, Bw. Sachidanund Ramparsad, Kiongozi wa PsW Rwanda, Bw. Mwangi Karanja, na Mtaalamu wa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa Sekta ya Umma (International Public Sector Accounting Standards-IPSAS) kutoka Zimbabwe, Bw. Amon Dhliwayo (hawapo pichani).

Alisema kuwa Tanzania ilikuwa nchi ya mwanzo kabisa katika Bara la Afrika kutumia viwango hivyo vya kimataifa vya uhasibu, hatua iliyochangia nchi kuwa na taarifa za fedha zenye viwango na zinazokubalika kimataifa.

Aliziasa nchi nyingine kufuata nyayo za Tanzania na baadhi ya nchi nyingine za Afrika, kutumia mfumo huo wa usimamizi wa fedha za umma unachangia taarifa za fedha kuwafikia wananchi na hivyo kuchangia maendeleo ya nchi.
Baadhi ya wahasibu na wataalamu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Wahasibu wa Serikali barani Afrika, wakifuatilia kwa umakini mjadala uliosimamiwa na Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Tanzania, CPA. Leonard Mkude (hayupo pichani), kuhusu namna Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa Sekta ya Umma (International Public Sector Accounting Standards-IPSAS) vinavyoweza kuchochea msukumo wa kisera na kutumia Uhasibu wa Ujumuishaji kwa Uboreshaji wa Usimamizi wa Mali na Madeni, wakati wa Mkutano wa Tatu wa Jumuiya ya Wahasibu wa Serikali barani Afrika, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Accra (AICC), nchini Ghana.

Kwa upande wake, Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Tanzania, CPA Leonard Mkude, alisema kuwa matumizi ya viwango vya kimataifa wa uhasibu wa fedha za Umma (IPSAS), umekuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa usimamizi na udhibiti wa fedha za umma umekuwa wa kiwango kikubwa, zinawekwa wazi na kujadiliwa na makundi mbalimbali ikiwemo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vinachochea msukumo wa kisera na kutumia Uhasibu wa Ujumuishaji kwa Uboreshaji wa Usimamizi wa Mali na Madeni.
Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Tanzania, CPA. Leonard Mkude (wa kwanza kulia), Mtaalamu wa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa Sekta ya Umma (International Public Sector Accounting Standards-IPSAS) kutoka Zimbabwe, Bw. Amon Dhliwayo (wa pili kulia), Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mauritania, Bw. Sachidanund Ramparsad (wa pili kushoto) na Kiongozi wa PsW Rwanda, Bw. Mwangi Karanja ( wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutamatika kwa mjadala wao uliozungumzia namna Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa Sekta ya Umma (International Public Sector Accounting Standards-IPSAS) vinavyoweza kuchochea msukumo wa kisera na kutumia Uhasibu wa Ujumuishaji kwa Uboreshaji wa Usimamizi wa Mali na Madeni, wakati wa Mkutano wa Tatu wa Jumuiya ya Wahasibu wa Serikali barani Afrika, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Accra (AICC), nchini Ghana.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Accra-Ghana).

Mkutano huo uliobeba Kaulimbiu isemayo “Afrika ya Kesho: Kuimarisha Usimamizi wa Fedha za Umma kwa ajili ya Ustawi wa Kiuchumi", umewahusisha washiriki zaidi ya 2,000 kutoka nchi 55 za Afrika, umelenga kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kusimamia matumizi sahihi ya fedha za umma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news