JESHI la Polisi lingependa kutoa taarifa baada ya saa 24 kupita toka tulipotoa taarifa ya mwisho asubuhi ya tarehe 11.12.2025 juu ya hali ya usalama nchini.
Tungependa kuwajulisha kuwa, kwa ushirikiano wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na nyinyi wananchi na wadau wengine katika kutimiza jukumu la pamoja la kulinda amani, utulivu na usalama nchini, hadi sasa nchi yetu kiusalama ni shwari na shughuli za kiuchumi na za kijamii ziliendelea vizuri katika mazingira ya amani kwa kipindi hicho cha masaa 24.
Tunapoelekea kwenye siku za mwisho wa wiki, tunazidi kutoa wito kwa kila mmoja wetu, kuendelee kutii sheria sambamba na kushirikiana kwa kila mmoja na nafasi yake, kulinda na kuimarisha amani kwani kila mmoja wetu anaihitaji katika maisha na katika shughuli zetu za kila siku.
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vinaendelea kuwaahidi tutaendelea kulinda usalama wa nchi yetu sote, maisha na mali za kila mmoja ndani ya Taifa letu la Tanzania.
Aidha, tuendelee kuelimishana na kuhimizana kuyakataa yale yote yanayo hamasishwa kwa njia mbalimbali na katika maneno ya kubadilisha mbinu kila mara ili kutaka kutuchonganisha na kutujengea chuki kati yetu lengo lao likiwa ni kutuingiza katika vurugu ambazo matokeo yake siyo mazuri kama tunavyo shuhudia katika maeneo mengine duniani.
Imetolewa na;
Dodoma,Tanzania

