IRINGA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, limeona picha mjongeo inayosambazwa katika mitandao ya kijamii akionekana Askari wa Polisi Usalama wa Barabarani akishawishi rushwa.
Askari huyo kwa msaada wa picha hiyo amepatikana na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake.
Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Iringa.
