DAR-Naibu Mkuu wa Taasisi Mipango, Fedha na Utawala, Dkt. Zena Mnasi Mabeyo akipokea tuzo ya Uandaaji wa Hesabu kwa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu wa Sekta ya Umma (International Public Sector Accounting Standards (IPSAS), kundi la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania.
Katika tuzo hizo Chuo cha Ustawi wa Jamii kimeibuka mshindi wa tatu,ikiwa ni mara ya nane mfululizo toka mwaka 2017 ambapo ISW inashika nafasi za juu kwenye mashindano hayo.







