DPP awafutia mashtaka ya uhaini Niffer na Mika Chavala

DAR-Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) imewafutia mashtaka ya uhaini na uchochezi mfanyabiashara Jennifer Jovin maarufu Niffer, na Mika Chavala waliokamatwa kutokana na vurugu za Uchaguzi Mkuu, Oktoba mwaka mkuu.
Hatua hiyo imekuja wakati Tume ya Uchunguzi wa vurugu hizo iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan ikiendelea na kazi hiyo.

Ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa wamefurika katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Jumatano Desemba 3, 2025 walilipuka kwa vilio vya furaha wakati ilipotangazwa kuwa wawili hao wameachiwa huru.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya DPP kuwasilisha ombi mahakamani la kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi dhidi ya Niffer na Chavala, ambapo Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamua, alikubaliana na ombi hilo la upande wa Jamhuri na kutangaza rasmi kuwaachia huru.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka gerezani, Niffer aliishukuru familia yake, mamlaka mbalimbali na Rais Samia, akisema bado anaendelea kuelewa kilichotokea lakini anafurahi kuachiwa huru.

Wawili hao walikuwa wanakabiliwa na kesi namba 26388/2025 chini ya kifungu cha 92(1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai, Sura ya 20, marejeo ya mwaka 2023, wakihusishwa na vurugu za maandamano wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Aidha,Wakili wa utetezi, Peter Kibatala, alisema DPP ametumia madaraka yake ipasavyo na kwamba hatua hiyo imefungua ukurasa mpya, ingawa sheria haimlazimishi kueleza sababu za kufuta mashtaka hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news