Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa apokea Ujumbe Maalum wa Rais Dkt.Samia

NEW YORK-Ujumbe kutoka kwa Mheshimiwa António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Desemba 14  2025, wakati wa kupokea Ujumbe Maalum kutoka Tanzania.
“Tanzania imekuwa rejea na mfano wa kuigwa katika masuala ya amani na mshikamano wa kijamii barani Afrika na duniani kote,” alisema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, alipokuwa akipokea Ujumbe Maalum.

Sifa ya Tanzania kama kinara wa amani ilijaribiwa katika uchaguzi wa hivi karibuni uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025, lakini taifa lilifanikiwa kuvuka jaribio hilo la kwanza kwa mafanikio.

“Umoja wa Mataifa ungependa kuona Tanzania ikiendelea kubaki kuwa taifa lenye umoja na mfano bora wa kuigwa,” alisema Katibu Mkuu Guterres alipokuwa akipokea Ujumbe Maalum uliobeba ujumbe kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Kombo, pamoja na ujumbe wake.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mazungumzo ya kitaifa yenye maana na jumuishi ili kushughulikia chanzo cha matukio ya vurugu yaliyotokea tarehe 29 Oktoba, pamoja na kuweka mikakati ya kuyatatua na kuyazuia yasijirudie tena.

Aidha, aliahidi msaada kamili wa Umoja wa Mataifa kabla na baada ya Tume ya Uchunguzi iliyoundwa nchini Tanzania kukamilisha majukumu yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here