Magazeti leo Desemba 11,2025

OBADIA Mpenzu (22), mkazi wa Kitongoji cha Majimoto, Kijiji cha Nanyala, Wilaya ya Mbozi, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumjeruhi bibi yake, Tabia Sengo (80).
Akizungumza kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanyala, Maneno Mwambunga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa lililotokea usiku wa Desemba 8, 2025.

Alisema mtuhumiwa alitekeleza tukio hilo la ukatili baada ya kufika nyumbani kwa bibi yake majira ya saa nne usiku ya Desemba 8,mwaka huu wakati mume wa bibi huyo akiwa kilabuni.
Mwambunga alisema,mara baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alikimbilia kusikojulikana ndipo uongozi wa kijiji ulianzisha msako uliodumu hadi asubuhi ya Desemba 9,2025. Ambapo majira ya saa tano walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa amejificha porini.

“Mtuhumiwa alikutwa akiwa amejificha porini na afya yake ilionekana kuwa dhaifu, akitapika na inadaiwa alikuwa amekunywa sumu kwa lengo la kujitoa uhai kwa kujutia kitendo alichofanya,”alisema Mwambunga.

Baada ya kumkuta na hali hiyo mtuhumiwa alikimbizwa katika Kituo cha Afya Nanyala kwa huduma ya dharura kabla ya kukabidhiwa polisi kwa ajili ya hatua zaidi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augostino Senga, alikiri kumshikiria mtuhumiwa huyo na kwamba hali yake inaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na uchunguzi utakapokamilika atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.














Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news