DAR-Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umetangaza kusitisha rasmi vibali vyote vilivyokuwa vikiruhusu baadhi ya magari kupita katika njia maalum za mabasi yaendayo haraka (BRT) kuanzia leo Desemba 10, 2025.
DART imeeleza kuwa,kuanzia sasa ni mabasi yaendayo haraka pekee ndiyo yanayoruhusiwa kutumia miundombinu hiyo, huku magari yote mengine yakitakiwa kutumia njia za kawaida.

