Tumaini Moshi (33) na Gaspar Mmari (24), wakazi wa Kinyerezi Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha na kujipatia vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh1.5 bilion mali ya Klabu ya The Voice Tz Limited.
Washtakiwa hao wamepandishwa kizimbani Desemba 11, 2025 na kusomewa shtaka lao na wakili wa Serikali, Frank Rimoy mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.
Mnamo Oktoba 29, 2025 eneo la Kinyerezi katika Klabu ya The Voice Tz Limited, washtakiwa kwa pamoja walifanya unyang'anyi wa kutumia silaha na kisha kuiba vitu vilivyokuwepo katika klabu hiyo.
Kabla ya kutekeleza wizi huo, Moshi na Mmari waliwatishia watu kwa kutumia mawe, fimbo na nondo ili waweze kujipatia vitu hivyo bila kipingamizi.
Moshi na Mmari, licha ya kukabiliwa na kesi ya Jinai namba 28915 ya mwaka 2025 yenye shtaka moja la unyang'anyi wa kutumia silaha, wanakabiliwa na kesi nyingine ya uhaini mahakamani hapo, ambapo ipo katika hatua ya kutajwa. Kesi yao ya unyang'anyi wa kutumia silaha imeahirishwa na itatajwa tena Disemba 22, 2025.
















Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo














