Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu, imekutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila na kujadili mambo mbalimbali yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi huo.
Kikao hicho kilifanyika Desemba 18, 2025 kwenye ofisi za muda za tume hiyo jijini Dar es Salaam, ambapo Chalamila aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam.Tume hiyo chini ya uenyekiti wa Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman, imeundwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ikiwa na wajumbe wengine saba ambao ni Watanzania wabobezi katika masuala mbalimbali.
Majukumu ya tume hiyo ni pamoja na kuchunguza chanzo cha matukio ya Oktoba 29, mwaka huu, kubaini waliohusika, kutathmini madhara yaliyojitokeza na kupendekeza hatua za kuimarisha amani, usalama na umoja wa kitaifa.
Tume imewaita wananchi watoe taarifa, ushahidi, maoni na mapendekezo yatakayosaidia katika uchunguzi wake.
Kwa mujibu wa Jaji Mkuu mstaafu Chande, mafanikio ya kazi hiyo yatategemea ushirikiano wa wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia kubainisha ukweli.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo









.jpeg)


