Kamati ya Ushauri wa Kisheria Mkoa wa Tanga imefanikiwa kusuluhisha mgogoro wa Ardhi kati ya Kampuni ya Mafuta ya Lake Oil Company Limited na Bi. Christine Malongo Muller (ambaye ni Mjane wa Marehemu Rudolf Muller).

Kamati ya Ushauri Mkoa wa Tanga ikiongozwa na Mwenyekiti wake Wakili wa Serikali Mkoa wa Tanga, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Rebbeca Msalangi imefanikiwa kusuluhisha mgogoro huo uliodumu kuanzia mwaka 2019 hadi 2025 ukihusisha Shamba lililopo eneo la Mkuzi, Wilayani Lushoto Mkoani Tanga.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






















