WATENDAJI wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na wenzao wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wamekutana na kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa utendaji hususani katika usimamizi wa masuala ya kikodi yanayotokana na huduma zinazodhibitiwa na EWURA.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Gerald Maganga amesema EWURA ni mshirika mzuri katika kuisaidia TRA kutekeleza wajibu wake wa usimamizi wa kodi nchini.“Ushirikiano uliopo kati ya taasisi hizi mbili, utatupeleka mbele, tuudumishe na tusimamie utekelezaji wa makubaliano yetu,”amesema.
Meneja wa TRA mkoa wa Dodoma, Pendolake Elinisafi ameishukuru EWURA kwa kuipatia TRA ushirikiano mzuri, na kuahidi kuuendeleza ili kuweka msingi imara wa mafanikio ya taasisi hizo mbili na taifa kwa ujumla.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo













