Magazeti leo Desemba 30,2025

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo ameliagiza Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Yustino Mgonja kutumia utaalamu na timu yake kukamata mara moja kundi la watu waliofanya mauaji ya Mzee Salehe Idd Salehe.
Salehe ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Zavala, Kata ya Buyuni wilaya ya Ilala Dar es salaam alivamiwa akiwa nyumbani kwake na kundi la wahalifu Desemba 4, 2025 saa 11:00 alfajiri na alifariki siku hiyo akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Amana.

Mpogolo ametoa agizo hilo wiki iliyopita kwenye mkutano wake na wananchi uliofanyika katika Mtaa wa Zavala baada ya kupata taarifa za uvamizi wa kinyama aliyofanyiwa mzee huyo akiwa nyumbani kwake na baadaye kusababisha kifo chake.

Akizungumza katika mkutano huo Mpogolo amesema mzee Salehe katika maisha yake amekuwa mzalendo wa kweli kwa kupigania maeneo ya wazi ya serikali mfano shule, masoko na vituo vya afya yasichukuliwe na genge la wahalifu wanaouza maeneo hayo ya viwanja vilivyopimwa na serikali katika Programu ya Viwanja 20,000 Kata ya Buyuni kati ya miaka ya 2003/2005.

“Kamanda RPC wa Ilala nakuagiza tumia vyombo vyako na utaalamu wako na ninahakika unaweza kuakikisha mnawakamata watu wote waliofanya mauaji haya na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Kwa kuwa wauaji hawa inaelekea wanao mtandao mkubwa wa kiuhalifu katika eneo letu la Wilaya za kipolisi za Chanika na Ukonga,” alisema Mpogolo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news