Naibu Waziri Maghembe apokea Nakala za Utambulisho za Balozi Mteule wa Namibia nchini Tanzania

DODOMA-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Namibia nchini, Mhe. Gabriel Sinimbo, katika tukio lililofanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma, Desemba 10, 2025
Katika mazungumzo yao, Mhe. Dkt. Maghembe amempongeza Mhe. Sinimbo kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo ya kuiwakilisha nchi yake hapa Tanzania na kumhakikishia ushirikiano kutoka Wizarani na Serikalini kwa ujumla wakati wote atakapokuwa akitekeleza majukumu yake ya Ubalozi hapa nchini.
Kwa upande wake, Balozi Mteule, Mhe. Sinimbo amemshukuru Mhe. Maghembe kwa mapokezi mazuri na kueleza dhamira ya Serikali ya Namibia ya kuendelea kukuza ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya mataifa haya mawili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news