Jeshi la Polisi Tanzania limemkamata na lina mshikilia Thadey Sabinus Kweka, mwenye hati za kusafiria namba C23858350 tarehe 28.12.2025 majira ya usiku huko mkoani Kilimanjaro.
Mtuhumiwa huyu amekamatwa kutokana na tuhuma za jinai zinazo mkabili mojawapo ikiwepo uchochezi ambao ni kinyume na sheria za nchi.
Taratibu za kukamilisha ushahidi ikiwa ni pamoja na kupata maelezo yake juu ya tuhuma hizo unaendelea ili hatua nyingine za kisheria ziweze kufuata.
Imetolewa na;
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
