Rais Dkt.Mwinyi aongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Disemba 29,2025 ameongoza Kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi (BLM) katika kipindi cha pili cha Serikali ya Awamu ya Nane.
Kikao hicho kimefanyika Ikulu, Zanzibar, na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Katika kikao hicho, kilichofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Mapinduzi, Rais Dkt. Mwinyi pia ameongoza hafla ya uapisho wa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe. Mgeni Khatibu Yahya, aliyeteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo.
Kabla ya uteuzi wake, Mhe. Mgeni Khatibu Yahya alikuwa akihudumu kama Mkuu wa Wilaya ya Chakechake, Pemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news