ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Naibu Makatibu Wakuu wapya katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 16,2025 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Mhandisi Zena A. Said.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa,uteuzi huo umeanza rasmi tarehe 15 Desemba 2025, huku walioteuliwa wakitarajiwa kuapishwa Jumatano, tarehe 17 Desemba 2025 saa 8:00 mchana, Ikulu Zanzibar.

