Rais Trump asema viongozi wa Ulaya ni dhaifu

WASHINGTON DC-Rais wa Marekani Donald Trump amewakosoa viongozi wa Ulaya kwa kuwaita dhaifu huku akibainisha kuwa, Marekani inaweza kupunguza msaada kwa Ukraine.
Trump ameyasema hayo katika mahojiano ya kina na mtandao wa habari wa Politico ambapo amesisitiza kuwa, mataifa hayo dhaifu yameshindwa kudhibiti uhamiaji au kuchukua hatua madhubuti kukomesha vita vya Ukraine na Urusi, akiwatuhumu kwa kuiacha Kyiv ipigane hadi ianguke.

Aidha,Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Yvette Cooper amesema, anachokiona barani Ulaya ni uimara huku akitoa mfano wa uwekezaji katika ulinzi pamoja na ufadhili kwa Ukraine.

Cooper alimgeukia Rais wa Urusi, Vladimir Putin kwa kudai hadi sasa ansendelea kuzidisha mgogoro huo kwa kutekeleza mashambulizi zaidi ya ndege zisizo na rubani na makombora huko Kyiv.

Pia, Rais Trump aliendelea kuongeza shinikizo kwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuunga mkono makubaliano ya amani, na kuwa tayari kutoa ushirikiano kwa kukabidhi eneo kwa Urusi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here