Sekta ya Utalii Tanzania yarekodi mafanikio makubwa

NA DIRAMAKINI

SEKTA ya Utalii nchini Tanzania imepata mafanikio makubwa kimataifa chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameifanya sekta hiyo kuwa nguzo muhimu ya uchumi wa taifa, diplomasia ya kimataifa na utambulisho wa nchi duniani.
Tangu aingie madarakani, Rais Dkt.Samia ameweka mkazo maalum katika utalii wa kimkakati unaotumia rasilimali za asili, urithi wa kitamaduni na diplomasia ya kiuchumi kama nyenzo za kuipaisha Tanzania katika soko la utalii la dunia.

Juhudi hizi zimeongeza idadi ya watalii wa kimataifa na mapato yatokanayo na sekta hiyo, pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi.

Hatua mojawapo iliyobeba uzito mkubwa ni uzinduzi wa kampeni ya kimataifa ya kuitangaza Tanzania kupitia filamu ya “The Royal Tour”, ambayo Rais Samia alishiriki yeye binafsi.

Filamu hiyo iliitangaza Tanzania katika majukwaa makubwa ya kimataifa kwa kuonesha vivutio vikuu ikiwemo Hifadhi ya Taifa Serengeti, Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro, fukwe za Zanzibar na urithi wa kitamaduni wa jamii za Kitanzania.

Kampeni hiyo imeongeza kwa kiasi kikubwa mwonekano wa Tanzania kama kivutio salama, cha kipekee na cha kiwango cha juu duniani.

Aidha, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji katika sekta ya utalii, kwa kuboresha miundombinu ya usafiri, huduma za viwanja vya ndege, hoteli na hifadhi za taifa.

Hatua hizi zimeongeza imani ya wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, na kuchochea ukuaji wa utalii wa kisasa na endelevu.

Ni kwa juhudi hizi za Rais Dkt.Samia ambapo Tanzania imekalia kiti cha enzi cha World’s Leading Safari Destination 2025 katika tuzo zilizotolewa hivi karibuni Bahrain.

Sio bahati. Ni matokeo ya urithi wa taifa lililobarikiwa na kutunzwa, hifadhi zisizo na mfano, na uzoefu wa safari ambao dunia nzima inauonea wivu.

Serengeti imetangazwa kuwa Mbuga bora ya wanyama 2025, mahali ambapo uhamaji wa wanyamapori unaandika historia hai kila mwaka.

Wakati huo huo, Zanzibar yenye fukwe za kuvutia inang’ara kama kituo kinachoongoza Afrika, ikichanganya biashara, starehe, na utamaduni kwa hadhi ya kimataifa.

Huu ni ujumbe kwa dunia. Tanzania siyo mahali pa kutembelea tu. Ni uzoefu wa kuishi, kuona, na kukumbuka milele.

Safari bora duniani zinaishi hapa na hata baada ya hali ya sintofahamu kisiasa, sekta ya utalii imeibuka kwa kasi ya kipekee kuaksi jinsi dunia inavoipenda hii nchi yetu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news